UTANGULIZI
Chama Kikuu cha Ushirika Cha Kahama (KACU) LTD Kiliandikishwa tarehe 20.04.1994 chini ya Sheria ya Vyama vya Ushirika namba 15 ya Mwaka 1991 fungu la 30 kwa Usajili namba 5493.
KACU LTD ina jumla ya Vyama Wanachama 126, ambapo Vyama 46 vinajishughulisha na kilimo cha zao la Tumbaku, Vyama 66 zao la Pamba na Vyama 14 vinajishughulisha na mazao yote mawili ya Pamba na Tumbaku. KACU LTD ina jumla ya wakulima 13,455 kutoka kwenye Vyama vya msingi ambavyo ni wanachama wa KACU LTD.
DHUMUNI KUU
Kustawisha hali ya Uchumi ya Wanachama kwa kufanya mipango ya kuendeleza shughuli za kilimo cha zao la Tumbaku, Pamba na mazao mengine zinazoendeshwa na Vyama vilivyojiunga nacho kwa hiari na kufuata misingi na taratibu za Vyama vya Ushirika
DIRA YA CHAMA
KACU LTD Kuwa chama kikuu cha Ushirika kinachotoa Usimamizi Madhubuti na Weledi katika Vyama wanachama na jamii ili kuboresha viwango vya Kiuchumi vya Wakulima na maendeleo ya jamii katika Wilaya ya Kahama
DHIMA YA CHAMA
Kuboresha Uzalishaji wa Mazao miongoni mwa Vyama wanachama kwa kutoa mafunzo endelevu kwa ajili ya uendeshaji mahiri wa KACU LTD na Vyama wanachama wake
MISINGI YA CHAMA (CORE VALUES)
Ushirikiano/Mshikamano(Solidarity: Lengo ni Kuboresha muundo wa watendaji wa kahama cooperative union Mafanikio ya Chama yatafikiwa endapo kutakuwepo na ushirikiano na mshikamano wa karibu kati ya wanachama, Bodi watendaji na wadau wengine. Ni wajibu wa kila mdau kutoa Ushirikiano pale inapohitajika kufanya hivyo.
Uwajibikaji (self-responsibility): Viongozi wa chama, Wanachama na watendaji wanapaswa kuwajibika kwa masilahi mapana ya Chama.
Kujaliwanachama: Mara zote Viongozi wa chama pamoja na watendaji watapaswa kutoa huduma iliyo bora kwa wanachama wake.
Uwazi:Shughuli za Chama zitaendeshwa katika hali ya uwazi kwa kuzingatia misingi ya kumlinda mwanachama (consumer protection) pamoja na kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya chama.
Ustadi:Bodi pamoja na watendaji watapaswa kuzingatia na kufuata viwango vya kitaalamu walivyonavyo wakati wa kuendesha shughuli za Chama.
Uaminifu (Honesty):Viongozi wa chama pamoja na watendaji wanapaswa kuwa waaminifu wakati wa kuendesha shughuli za Chama.
Kujitoleanakujitegemea(self-help):Viongozi wa chama na watendaji wanahamasishwa kuwa na moyo wa kujitolea na kujitegemea wakati wote kwa manufaa ya Chama na wanachama wake.
MIPANGO YA CHAMA
- Kuhakikishaupatikanajiwapembejeo bora nakwawakatikwavyamawanachamawa KACU
LTD. - Kuhakikishaupatikanajiwahuduma bora zauganikwawakulimawavyamawanachamawa
KACU LTD - Kuhakikishaupatikanajiwamasokoyauhakikanabei bora
yamazaoyanayozalishwanawakulima. - Kusimikamitamboyakukamuamafuta,
mtambowakutengenezasabuninamtambowakutengenezamkaa. - Kuhakikishauendelevuwamafunzonakuwajengeauwezoviongoziwavyamavyaushirika,
kutiisheria, kanunizachamakikamilifunakuongezamatumiziya Tehama.
MAFANIKIO YA KACU LTD
- Kuongeza idadi ya wanachama kutoka vyama waanzilishi 32 hadi kufikia vyama
wanachama 126. - Kuhakikisha Pembejeo za kilimo zinawafikia wakulima kwa wakati na kutoa huduma
bora za ugani kwa wanachama wa KACU LTD. - Kufufua kiwanda cha kuchakata Pamba na kuongeza vyerehani vipya 8.
- Kusimamia ununuzi wa viuatilifu vya zao la Pamba nchi nzima kwa niaba ya Bodi ya
Pamba kwa misimu mitatu mfululizo. - Kuwa chama kikuu cha mfano katika usimamizi na uongozi.
- Kupata hati safi ya ukaguzi kwa miaka miwili mfululizo 2019/2020 na 2020/2021