bopen

Chama kikuu cha ushirika cha kahama (kacu ltd) chalipa malipo ya pili kwa wakulima wa zao la pamba.

Kahama.

Chama Kikuu cha Ushirika cha Kahama (KACU) LTD  kimekabidhi mfano wa hundi kwa wakuu wa Wilaya ya Kishapu, Kahama na Nyanhwale ikiwa ni malipo ya pili ya wakulima wa zao la pamba. Jumla ya Shilingi za kitanzania Milioni tisi mia nne arobaini na sit amia tano ishirini  (TZS 90,446,520/=) zitatimika kulipa malipo ya pili ambapo kila kilo iliyonunuliwa italipwa Tzs 40/=

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi mfano wa hundi kwa wakuu wa wilaya za Kahama, Kishapu na Nyanh’wale Mwenyekiti wa chama kikuu cha Ushirika Kahama Bw. Emmanuel P. Cherehani alisema, Jambo hili limewezekana kutokana na faida iliyopatikana baada ya kuuza bidhaa zilizozalishwa (pamba nyuzi na mbegu) zilizotokana na pamba iliyonunuliwa kutoka kwa wakulima wanachama KACU LTD na wasiokuwa wanachama na hii ndio maana halisi ya Ushirika kuwajali wakulima.

Bw. Cherehani aliendelea kusema KACU LTD imechangiza ongezeko la bei ya pamba kutoka TZS 810/= kwa kilo iliyokuwa ikilipwa na makampuni binafsi kwenye maeneo mengi hadi kufikia TZS 920/= hali iliyopelekea mkulima kunufaika na bei inayoridhisha. Malengo yaliyopo kwa msimu 2020/2021 ni Kununua vyerehani vipya 11 ili kuongeza uwezo wa uzalishaji wa kiwanda na Kununua pamba kilo 6,000,000 (milioni sita) kutoka kwa wakulima wa Wilaya za Kahama, Nyang’hwale, Kishapu na maeneo mengine.

Kwa upande wa wakuu wa Wilaya za Kahama, Kishapu na Nyanh’wale walikishukuru chama  kikuu cha ushirika cha Kahama KACU LTD kwa kurudisha faida iliyopatikana kwa wakulima.

MWISHO.

About "kacu"

No Comments

Leave a Reply