Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amekabidhi gari mbili (2) aina ya Tata zenye uwezo wa tani 25 kila moja na zenye thamani ya Tzs. Milioni 380 kwa Chama Kikuu cha Ushirika cha Kahama (KACU LTD) kutoka kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kwa lengo la kuboresha shughuli za uzalishaji wa zao la pamba na utoaji huduma kwa wateja wao ambao ni wakulima na wananchi.
Awali akitoa salamu za Benki, Afisa Mikopo kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Ndugu Andrew Ezekiel amesema kuwa hawana hofu kabisa na KACU katika utekelezaji wa majukumu yao huku akiwaasa kuwa na uangalizi na usimamizi mzuri na wa karibu zaidi ili kuhakikisha kiwanda cha KACU kinarudisha thamani na heshima ya zao la Pamba.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya KACU LTD Ndugu Emmanuel Nyambi ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Kilimo kwa kuwapatia gari hizo kwani zitawasaidia kwenye uzalishaji na kuongeza thamani ya zao la Pamba kwa wanachama wao na kuongeza pato lao na Serikali kwa ujumla


No Comments