bopen

TANGAZO LA ZABUNI

TANGAZO LA ZABUNI MBALIMBALI MSIMU 2026/2027

  1. Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) LTD kimetenga Fedha kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za kiwanda katika kata ya Mhongolo Manispaa ya Kahama. Hivyo kwa tangazo hili Meneja Mkuu wa KACU LTD anawatangazia watu wote wenye uwezo wa kutoa Huduma/Bidhaa mbalimbali kufika ofisi za KACU kuchukua zabuni (Nukuu za bei) zitakazowaongoza kujaza na kuleta maombi yao katika Ofisi za KACU zabuni kwa ajili ya msimu 2026/2027.
  • Wazabuni wenye nia ya kutoa huduma/kufanya kazi na KACU LTD msimu 2026/2027 wanakaribishwa kuomba zabuni na kupatiwa nyaraka za zabuni (nyaraka zipo kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili) kwenye ofisi ya ugavi kuanzia saa 2:00 Asubuhi hadi saa 10:00 Alasiri siku za kazi jumatatu hadi ijumaa isipokuwa siku za sikukuu za kitaifa.
  • Zabuni zinazohitajika/zinazotangazwa ni Pamoja na;
  1. Zabuni ya vifungashio vya pamba yenye zabuni na. KACU/2026/2027/G/GINNERY inayojumuisha magunia ya kubebea pamba, vitambaa vya kufungia robota na Nyaya za kufungia robota. (Ada ya zabuni ni Tsh. 200,000/=)
  1. Zabuni ya vifungashio vya mafuta yenye zabuni na. KACU/2026/2027/G/OIL inayojumuisha vifungashio vya kubebea mafuta ya kula (Ada ya zabuni ni Tsh. 200,000/=)
  1. Zabuni ya Usafirishaji wa Pamba yenye zabuni na. KACU/2026/2027/S/TRANSPORT (Ada ya zabuni ni Tshs. 200,000/=)
  1. Zabuni ya Bima (Insurance Services) yenye zabuni na. KACU/2026/2027/S/INSURANCE (Ada ya zabuni ni Tsh 100,000/=)
  • Zabuni ya Collateral Management Services yenye zabuni na. KACU/2026/2027/S/COLLATERAL (Ada ya zabuni ni Tsh 100,000/=)
  • Zabuni ya Vipuri vya kiwanda (Factory Spare Parts) yenye zabuni na. KACU/2026/2027/G/SPARE (Ada ya zabuni ni Tsh 100,000)
  • Zabuni ya shajara (Books and Printings) yenye zabuni na. KACU/2026/2027/G/STATIONERY (Ada ya zabuni ni Tsh 100,000/=)

MASHARTI YA JUMLA NA MAALUM KWA WAOMBAJI WOTE

  1. Mwombaji alipe ada ya zabuni kupitia benki ya NMB A/C Na. 30603500023. Bank slip iwasilishwe ofisi ya malipo (Cash Office) kwa ajili ya kupata stakabadhi.
  • Mwombaji atatakiwa kuwasilisha barua halisi (original) ya maombi ya zabuni anayoomba na aambatanishe leseni ya biashara husika/ Vivuli vya VAT, Valid Tax Clearence Certificate na TIN, nakala halisi ya stakabadhi ya malipo ya ada ya zabuni na nyaraka nyingine zinazotambulisha uhalali wa mwombaji/ kazi yake.
  • Waombaji wenye makampuni waambatanishe nyaraka zote muhimu za kampuni.
  • Kwa vifaa vilivyoainishwa kwa neno “sampuli” waombaji itabidi wafike KACU LTD ili waone sampuli zinazohitajika.
  • Nyaraka za zabuni zinapatikana kwa kuwasilisha stakabadhi ya ada ya zabuni (kulingana na zabuni inayoombwa) kwa Afisa ugavi wa KACU LTD, S.L.P 51 Kahama.
  • Kamati ya zabuni haitalazimika kumteua mzabuni aliyeomba kwa bei ndogo. Vigezo vilivyotolewa ndivyo vitasaidia kupatikana kwa mzabuni.
  • Maombi ya zabuni yawekwe kwenye bahasha iliyofungwa kwa lakiri (seal) yakiwa na nyaraka muhimu, rejea kipengere no 2, Zabuni zote ziwekwe kwenye sanduku la zabuni lililopo katika ofisi ya Afisa Ugavi. Zabuni iandikwe zabuni inayoombwa; Zabuni zitumwe kwa Meneja Mkuu, KACU Ltd S.L.P 51 Kahama.
  • Mwisho wa kupokea maombi ya zabuni ni siku ya Ijumaa tarehe 22 Mei, 2026 saa 4;00 Asubuhi na mara baada ya kusitisha zoezi hilo Zabuni zitafunguliwa Tarehe 22 Mei, 2026 saa 4:30 Asubuhi kwenye ofisi ya Meneja Mkuu, waombaji /wawakilishi wanakaribishwa kuhudhuria ufunguzi.
  • Zabuni zilizochelewa hazitafunguliwa na kusomwa mbele ya hadhara kwenye sherehe ya ufunguzi.

ABDUL ALLY

MENEJA MKUU

KACU LTD

About "kacu"

No Comments

Comments are closed.